1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Hatuna silaha za kutosha kuikomboa Mariupol

Sylvia Mwehozi
12 Aprili 2022

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake haina silaha za kutosha zinazohitajika kuweza kuukomboa mji wa Mariupol ambao upo hatarini kudhibitiwa na vikosi vya Urusi.

https://p.dw.com/p/49o1b
Ukraine | Kriegseindrücke aus Mariupol
Picha: Alexander Ermochenko/REUTERS

Zelenskiy ametoa kauli hiyo kupitia hotuba kwa njia ya vidio akitaka ulimwengu kumsaidia silaha kama vile mizinga na ndege za kivita ili kuweza kuhimili mashambulizi ya Moscow. Amedai kwamba Urusi inaweza kutumia silaha za kemikali nchini Ukraine na kuzitaka nchi za Magharibi kuiwekea Moscow vikwazo vikali. 

Kiongozi wa eneo linalotaka kujitenga la Donetsk Denis Pushilin alinukuliwa Jumatatu jioni akisema kwamba mji wa Mariupol tayari umeangukia mikononi mwa wanajeshi wa Urusi. Hata hivyo kamanda wa kikosi cha wanajeshi wa Ukraine Valerii Zaluzhnyi alisema kuwa mtandao unaounganisha wanajeshi wanaolinda Mariupol bado haujakatika. Wapiganaji wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipigana kwa wiki kadhaa wakiunga mkono jeshi la Urusi kuweza kuudhibiti mji wa kimkakati wa Mariupol. 

Ukraine | Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Urusi Volodmyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa/picture alliance

Zaidi ya raia 10,000 wameuawa Mariupol

Meya wa mji wa bandari wa Mariupol amesema zaidi ya raia 10,000 wamefarikikatika mzingiro wa Urusi kwenye mji huo, na kwamba idadi ya vifo inaweza kupindukia 20,000 kutokana na miili "iliyotapakaa mitaani". Akizungumza kwa njia ya simu na shirika la habari la Associated Press, Meya Vadym Boychenko amedai kwamba vikosi vya Urusi vilipeleka vifaa vya kuchoma maiti katika mji huo vilivyowasili katika mfumo wa magari. Aidha Boychenko pia amevituhumu vikosi vya Urusi kwa kuzuia misafara ya misaada ya kiutu katika jitihada za kuficha mauaji.

Madai hayo yametolewa wakati Urusi ikiripoti kuharibu mifumo kadhaa ya ulinzi wa anga ya Ukraine, katika kile kinachotajwa kama msukumo mpya wa kudhibiti anga na kuteketeza silaha ambazo Kyiv imezielezea kuwa muhimu kuelekea mashambulizi mapya ambayo yanatarajiwa upande wa mashariki. Watu takribani 4,300 wameweza kuhamishwa kutoka miji mbalimbali ya nchi kupitia njia salama za kiutu siku ya Jumatatu wakiwemo 556 kutoka mjini Mariupol.

Juhudi za diplomasia

Wakati huohuo Kansela wa Austria Karl Nehammer ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa Ulaya kuzuru Moscow na kukutana na Rais Vladimir Putin ameonyesha hali ya kukosa matumaini na juhudi za kidiplomasia katika kuutatua mzozo huo.

Ukraine | Pro Russisches Militärfahrzeug in Mariupol
Vikosi vinavyopigana kando na wanajeshi wa UrusiPicha: Chingis Kondarov/REUTERS

Akizungumza na waandishi wa habari Nehammer amesema kuwa "mazungumzo ya amani siku zote yanachukua muda mwingi huku mantiki ya kijeshi ikijielekeza moja kwa moja kwenye vita'", alimalizia Kansela huyo.

Baada ya mkutano wake na Putin, Nehammer alifanya mazungumzo na mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na kusisitiza umuhimu wa mikutano zaidi kama hiyo ili kuelezea moja kwa moja hasira ya Umoja wa Ulaya dhidi ya matendo ya urusi.Zelensky: Watu 100,000 waondolewa miji ya Ukraine

Wakati Nehammer akidai kwamba Urusi ina maslahi kidogo juu ya mkutano wa moja kwa moja na kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky, lakini Putin bado anayo matumaini na mazungumzo ya mjini Istanbul.

Ama kwa upande mwingine, Ufaransa imewafukuza maafisa sita wa Urusi wanaoshukiwa kufanya kazi kama majasusi chini ya ulinzi wa kidiplomasia baada ya idara za kijasusi za Ufaransa kufichua operesheni ya kisiri katika eneo lake.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ufaransa mnamo Aprili 4 kuwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi kama sehemu ya hatua ya pamoja ya Ulaya baada ya uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.