1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenski awasili Singapore kushiriki Jukwaa la Shangri-La

1 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewasili mjini Singapore kuhudhuria Jukwaa la Kimataifa la majadiliano ya usalama la Shangri-La, kusaka uungaji mkono wa kimataifa wakati Urusi ikiendelea kuishambulia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4gWvp
Singapore | Shangri-La
Zelenski awasili Singapore kushiriki Jukwaa la Shangri-LaPicha: Nhac Nguyen/AFP/Getty Images

Mwandishi  habari wa AFP alimuona rais Zelensky akiingia katika hoteli kunakofanyika mkutano huo unaohudhuriwa na mawaziri wa ulinzi kutoka mataifa kadhaa duniani.  

Rais huyo wa Ukraine amepangiwa kutoa hotuba mbele ya Jukwaa hilo kesho Jumapili. Zelesky amekuwa akifanya ziara barani Ulaya katika siku za hivi karibuni kuomba msaada zaidi wa kijeshi wa kupambana na mashambulizi kutoka Urusi. 

Mizozo ya Ukraine na Gaza yatawala Jukwaa la Shangri-La

Ziara yake imekuja baada ya uamuzi wa Marekani kuondoa vikwazo kwa muda vya utumiaji wa silaha zake kushambulia maeneo ya Urusi, hatua iliyokaribishwa na Zelensky. Urusi imeonya hatua hiyo itakuwa na taathira mbaya kwenye mzozo unaendelea.