1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR : Wapinzani wasusia kikao cha wawakilishi

12 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJO

Wawakilishi wa upinzani katika visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania hapo jana wamesusia kufunguliwa rasmi kwa Baraza la Wawakilishi na Rais Aman Abeid Karume wa visiwa hivyo.

Wawakilishi hao wamesisitiza kwamba wanasusia tu vikao vinavyohudhuriwa na Rais Karume kwa sababu wanaamini chama chake cha Mapinduzi CCM kimepora ushindi wao katika uchaguzi wa tarehe 30 mwezi wa Oktoba.

Akizungumza na shirika la habari la AFP mmojawapo wa wajumbe wa upinzani katika baraza la wawakilishi Abbasi Mhunzi amesema bado wanaedelea kusisitiza kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar yalitiwa mkono na kwamba upinzani utasusia shughuli zote zinazohudhuriwa na Karume.

Wajumbe 45 wa CCM walihudhuria kikao hicho ambapo Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho amesema anatafakari njia za kukabiliana na hali hiyo ya kususiwa kwa vikao.