1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yaagizia maelfu ya tani za mahindi kutoka Tanzania

19 Juni 2024

Zambia ina mpango wa kununua tani 650,000 za mahindi kutoka Tanzania, baada ya ukame kusababisha mapungufu katika kiwango cha uzalishaji nchini humo kwa zaidi ya asilimia hamsini.

https://p.dw.com/p/4hGJo

Haya yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano wa Zambia, Cornelius Mweetwa.

Waziri wa kilimo wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, Mtolo Phiri, hapo jana aliliambia bunge kwamba Zambia imesimamisha uuzaji wa mahindi nje kufuatia mapungufu ya tani milioni 2.1 na kwamba wangenunua nafaka hiyo ambayo ni chakula muhimu nchini humo.

Soma zaidi: Jinsi ya kuulinda udongo dhidi ya ukame

Uzalishaji wa mahindi nchini Zambia kwa mwaka wa 2023/2024 unatarajiwa kushuka na kufikia tani milioni 1.5 kutoka tani milioni 3.2.