1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 60 wahofiwa kufa katika vita kati ya makundi ya jihadi

21 Novemba 2023

Zaidi ya watu 60 wanahofiwa kupoteza maisha katika mapigano makali kati ya wapiganaji wa Boko Haram na kundi hasimu la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu la Mkoa wa Afrika Magharibi ISWAP.

https://p.dw.com/p/4ZErs
Jimbo la Nigeria la Borno I Boko Haram
Gari linalodaiwa kuwa la kundi la Dola la Kiislamu la Mkoa wa Afrika Magharibi ISWAP.Picha: Audu Ali Marte/AFP/Getty Images

Vyanzo vimeliambia shirika la habari la AFP kuwa, mapigano yalianza kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi baada ya wapiganaji wa ISWAP walipovamia boti za Boko Haram katika ziwa Chad linaloizunguka Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.

Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa waliokuwemo ndani ya boti hizo wakiwemo wavuvi na wanawake wa jamii ya Fulani waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram.

Makundi hayo mawili ya jihadi yameingia katika vita vikali vya kuwania mamlaka, huku kukiwa na mapigano makali kati yao tangu kundi la ISWAP lilipojitenga mwaka 2016.

Mapigano hayo yaliongezeka kufuatia kifo cha kiongozi wa Boko Haram mwaka 2021 wakati wa mapigano katika ngome ya msitu wa Sambisa.