1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHonduras

Zaidi ya watu 41 wamepoteza maisha kwenye jela, Honduras

21 Juni 2023

Zaidi ya watu 41 wamepoteza maisha kwenye jela moja ya wanawake nchini Honduras baada ya kuzuka kwa moto ulioteketeza sehemu ya gereza ambao chanzo chake ni uhasama baina ya magenge hasimu ya uhalifu.

https://p.dw.com/p/4Ss5L
Honduras | Gefängnisaufstand
Picha: Orlando Sierra/AFP

Inaarifiwa kwamba vurumai ilizuka kwenye gereza hilo lililo umbali wa kilometa 25 kaskazini mwa mji mkuu wa Honduras, Tegucigalpa baada wafungwa ambao ni wanachama wa genge la uhalifu kuingia kwenye moja ya vyumba vya wafungwa wa kundi lingine hasimu na kuwasha moto.

Manusura wamepelekwa hospitalini

Hadi sasa mbali ya vifo 41, wanawake wengine 5 wamejeruhiwa na wamepelekwa hospatali. Mamia ya ndugu na jamaa za wafungwa walikusanyika nje ya gereza hilo kutafuta taarifa kuhusu wapendwa wao. Haijafahamika iwapo wote waliopoteza maisha ni walikuwa wafungwa.