1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 30 wameuawa mashariki mwa Kongo

6 Aprili 2023

Zaidi ya watu 30 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mfululizo wa mashambulizi ya waasi wa ADF.

https://p.dw.com/p/4PnET
Demokratische Republik Kongo Soldaten
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Zaidi ya watu 30 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mfululizo wa mashambulizi ya waasi wa ADF. Hayo ni kulingana na Christophe Munyanderu, mratibu wa shirika la mkataba wa kuheshimu haki za binaadamu katika eneo hilo.Watu 5 wauawa katika shambulizi la majambazi mashariki mwa DRC

Munyanderu amesema wanaume, wanawake na watoto wameuawa na waasi wa ADF, kundi linalodai kuwa na mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, na kwamba mauaji hayo yalifanyika katika eneo lililo kati ya Irumu na wilaya ya Mambasa katika mkoa wa Ituri.

Hayo yanaripotiwa wakati viongozi wa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wale wa Uganda wanakutana mjini Beni ili kutathmini operesheni za pamoja dhidi ya kundi hilo la kigaidi la ADF ambalo limekuwa likisababisha maafa makubwa eneo hilo.