1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 20 wauawa katika vurugu za Darfur Magharibi

2 Januari 2020

Watu wapatao 24 wamethibitishwa kuuawa baada ya kambi ya kuhifadhi watu waliopoteza makazi nchini Sudan kuvamiwa jimbo la Darfur Magharibi

https://p.dw.com/p/3Vb2b
Sudan Darfur Konflikt Flüchtlinge
Picha: picture-alliance/AP Photo/K. Prinsloo

Kambi ya Krinding, ilivamiwa mnamo Desemba 29 hadi 30 kufuatia mzozo kati ya makundi ya asili ya Kiarabu na Kiafrika.

Kudumisha amani katika jimbo la Darfur pamoja na maeneo mengine ya Sudan ni moja wapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali mpya ya nchi hiyo tangu kuondoshwa madarakani raia wa zamani Omar al-Bashir.

Mgogoro mkubwa ulizuka Darfur mnamo mwaka 2003, baada ya waasi wengi wao waliokuwa sio wenye asili ya Kiarabu kupambana na serikali ya mjini Khartoum.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, watu wapato 300,000 waliuawa na wengine milioni 2.5 kupoteza makazi, ikiwa ni pamoja na watu 180,000 waliopoteza makazi Darfur Magharibi.