1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wahamiaji 1,400 Waafrika wawasili visiwa vya Canary

Josephat Charo
23 Oktoba 2023

Watu 321 walifika kisiwa cha El Hiero katika chombo kimoja na kupita rekodi ya awali ya boti moja kubeba watu 280 mnamo Oktoba 3.

https://p.dw.com/p/4XsrA
Spanien | Ankunft Migranten in El Hierro
Wahamiaji waafrika wakiwasili bandari ya La Restinga, El Hierro, visiwa vya Canary 21.10.2023Picha: Europa Press/ABACA/picture alliance

Zaidi ya wahamiaji 1,400 wa Kiafrika wamewasili katika visiwa vya Uhispania vya Canary wikendi hii, huku chombo kimoja kikiweka rekodi ya boti moja ya watu 321. Hayo yamesemwa na mamlaka za Uhispania jana Jumapili.

Katika taarifa yao iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, zamani Twitter, mamlaka za Uhispania zimesema jumla ya wahamiaji 1,457 walikuwa wamewasili katika visiwa hivyo nje ya pwani ya magharibi ya Afrika kati ya Ijumaa usiku na Jumapili asubuhi. Msemaji wa idara inayotoa huduma za dharura amesema wahamiaji wote waliowasili wanatokea barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.