1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wabunge 80 wa upinzani wajiuzulu, Pakistan

Jane Nyingi2 Oktoba 2007

Zaidi ya wabunge 80 wa upinzani nchini Pakistan wamejizulu bungeni hivi leo kupinga hatua ya rais Pervez Musharraf kugombea urais kwa kipindi kingine. Wabunge hao wameendea kusisitiza kuwa rais Musharraf hakubaliwi kushiriki katika uchaguzi huo wa urais utakaofanyika siku ya jumamosi.

https://p.dw.com/p/CH7J
Viongozi wa upinzani chini Pakistan katika mkutano mjini Islamabad.
Viongozi wa upinzani chini Pakistan katika mkutano mjini Islamabad.Picha: AP

Muda mfupi kabla ya wabunge hao kujiuzulu,mawakili wa upinzani walifanya juhudi za mwisho mwisho kumzuia Musharraf kushiriki katika uchaguzi huo , kwa kuiambia mahakama kuu nchini Pakistan kuwa kama mkuu wa majeshi Musharraf hastahili kuwa kugombea urais. Walipendekeza kuhairishwa kwa uchaguzi huo.

Musharraf ambaye ni rafiki mkubwa wa marekani kutoka taifa pekee la kiislamu linalounda silaha za kinuklia, anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo kufuatia kura kutoka za mabaraza mawili ya bunge la taifa na mabunge manne ya majimbo.

Japokuwa umaarufu wa Rais Musharraf umeendelea kudidimia, serikali tawala ya mseto inawingi wa wabunge,katika bunge linalotarajiwa kuvunjwa mwezi ujao kabla ya uchaguzi mkuu kati mwa mwezi januari. Musharraf wa umri wa miaka 64 ameahidi punde tu baada ya kuachaguliwa rais atangatuka madarakani kama mkuu wa majeshi tarehe 15 mwezi ujao.

Spika wa bunge la pakistan Chaudry Amir Hussain amethibitisha leo kupokea barua za kujizulu kutoka kwa wabunge 86 kati ya 342. Hakuna mbunge hata mmoja kutoka chama kikuu cha upinzani cha alikuwa waziri mkuu nchini humo Benazir Butto alikuwa miongoni mwa hao walioziuzulu.

Bhutto amekuwa akifanya mashauri ya mara kwa mara na Rais Musharraf kuhusu kugawana mamlaka,japokuwa pia amekuwa akipinga vikali hatua ya musharraf kugombea tena urais akiwa bado mkuu wa majeshi.

Amesema huenda hata wabunge kutoka chama chake wakaamua kujiuzulu hadi matakwa yake yatimizwe ya kuwepo kwa mabadiliko ya kidemocrasia nchini Pakistan. Bi Bhutto anataarjiwa kuamua mkakati wake katika mkutano wa chama hicho mjini London Uingereza hapo kesho.Hatua ya kujizulu kwa wabunge hao haitauchelewesha uchaguzi huo wa urais siku ya jumamosi hata kama chama cha Bhutto kitashiriki ila tu kitaufanya kutoaminiminika.

Katika kile kichoonekana kama pigo kubwa kwa upinzani wiki iliyopita mahakama kuu nchini Pakistan ilimruhusu Musharraf kubakia mkuu wa majeshi na vilevile kukitetea kiti cha urais.Baadaye tume ya uchaguzi nchini humo ilipuuzilia mbali malalamishi yao dhidi ya ugombezi wa Musharraf.

Hata hivyo wabunge wanaopmpiga Musharraf na wafuasi wa Butto waliwasilisha pingamizi mpya katika mahakama kuu dhidi ya musharraf dhidi ya Musharraf. Mpinzani wa karibu wa Musharraf katika uchaguzi huo wa urais ni Makhdoom Amin Faheem kutoka chama cha Bi Bhutto cha Pakistan Peoples party.Bhutto ameishi uhamishoni tangu mwaka 1999 badala ya kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi lakini wakati huu ameapa kurejea pakistan tarehe 18 mwezi huu.