1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Yunus awahakikishia wakimbizi wa Rohingya biashara muhimu

18 Agosti 2024

Serikali ya mpito ya Bangladesh imesema kuwa itawaunga mkono watu wa jamii ndogo ya wakimbizi warohingya walioko nchini humo katika kufanya biashara za bidhaa muhimu za kuuza nje ya nchi.

https://p.dw.com/p/4jbN2
Dhaka | Muhammad Yunus
Kiongozi mpya wa serikali ya mpito nchini Bangladesh, Muhammad YunusPicha: MUNIR UZ ZAMAN/AFP

Serikali ya mpito ya Bangladesh imesema kuwa itawaunga mkono watu wa jamii ndogo ya wakimbizi wa Rohingya walioko nchini humo katika kufanya biashara za bidhaa muhimu za kuuza nje ya nchi. Hayo yamesemwa na kiongozi mpya wa serikali ya mpito, Muhammad Yunus, hii leo katika hotuba yake kuu ya kwanza ya kisera tangu aingie madarakani.

Nchi hiyo ya Kusini mwa Asia ina takribani wakimbizi milioni moja ya warohingya. Wengi wao walikimbia nchi jirani ya Myanmar mwaka wa 2017 baada ya operesheni kali ya kijeshi, ambayo sasa inachunguzwa kama mauaji ya halaiki na mahakama ya Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi. Sheikh Hasina akabiliwa na shtaka la mauaji

Bangladesh ina viwanda 3,500 vya nguo vinavyochangia karibu asilimia 85 ya dola bilioni 55 katika mauzo ya nje ya kila mwaka.

Hivi karibuni baadhi ya kampuni zilihamisha uzalishaji nje ya nchi wakati wa machafuko yaliyomwangusha waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Sheikh Hasina.