1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Yellen "anatamani" kufanya kazi na China

16 Julai 2023

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema anatamani kufanya kazi na China katika masuala yaliyo na faida kwa pande zote mbili.

https://p.dw.com/p/4Txum
USA Finanzministerin Janet Yellen
Picha: SARAH SILBIGER/REUTERS

Ikiwa ni pamoja na marekebisho ya madeni kwa nchi masikini na kwamba benki za kimataifa za maendeleo zinahitaji mageuzi kabla ya ongezeko la mtaji kuzingatiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nchini India, kabla ya mkutano wa kundi la mawaziri wa fedha 20 na wawakilishi wa benki kuu, Yellen amesema ziara yake mjini Beijing wiki iliyopita ilisaidia kuweka uhusiano mzuri kati ya Marekani na China.

Soma pia: Yellen: Uhusiano wa China na Marekani uko katika mwelekeo sahihi

Aidha waziri huyo amesema Washington itaendelea kuzuia upatikanaji wa vifaa na teknolojia ya kijeshi kwa Urusi, ambayo Moscow inahitaji katika uvamizi wa Ukraine.

India, ambayo ni mwenyekiti wa mkutano wa G20 mwaka huu imeonyesha kwa kiasi kikubwa msimamo wa kutoegemea upande wowote kwenye vita hivyo na kukataa kuilamu Urusi kwa uvamizi huo. Pia imehimiza upatanishi wa kidiplomasia wakati ikiendelea kununua kwa wingi mafuta ya Urusi licha ya mataifa ya Magharibi kuibana Moscow.