1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON : Mkuu wa kijeshi ana afya nzuri na anaendelea kuongoza nchi kufuatia uvumi wa mapinduzi

28 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEgq

Mkuu wa kijeshi wa Myanmar Than Shwe yuko katika afya nzuri na katika uongozi wa nchi licha ya uvumi mkubwa kwamba amen’golewa madarakani au yuko mahtuti.

Waziri wa habari Birigedia Generali Kyaw Hsan ameuambia mkutano wa waandishi wa habari leo hii kwamba generali huyo mwenye umri wa miaka 73 yuko kwenye Ofisi inayoshughulikia Vita ambayo ni makao makuu ya baraza la kijeshi mjini Yangon.

Kutokana na uvumi kwamba kiongozi wa nchi hiyo Generali Mkuu Than Shwe amepinduliwa au amesafirishwa Singapore kwa matibabu Hsan amesema kwamba Shwe yuko katika afya nzuri na anaendesha shughuli zake za kuongoza nchi.

Amevishutumu vyombo vya habari vya kigeni katika kurepoti uvumi huo kwa kutowa habari za kichunguzi za uzushi ambazo hazina ukweli hata chembe.