1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi: Mataifa yenye nguvu fanikisheni amani Urusi na Ukraine

9 Julai 2024

Rais wa China Xi Jinping amemwambia waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban kwamba nchi zenye nguvu duniani zinapaswa kuzisaidia Urusi na Ukraine kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja.

https://p.dw.com/p/4i3PV
China | Viktor Orban na Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: China Daily via REUTERS

 Mwito wa huo wa rais Xi umetolewa wakati wa ziara ya kiongozi wa Hungary mjini Beijing iliyotajwa na kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya, kama ziara ya ujumbe wa amani. 

Ziara ya Orban China imefanyika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO unaoanza leo huko Washington, ambako suala la Ukraine linatarajiwa kugubika mazungumzo ya viongozi wa jumuiya hiyo.

Soma pia:Waziri Mkuu wa Hungary , Rais Xi Jinping wakutana Beijing

Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa  Marekani John Kirby amesema Marekani ina wasiwasi na mkutano kati ya Orban na rais Xi kwasababu ziara hiyo haionekani ikileta tija katika kujaribu kutafutia ufumbuzi vita vya Ukraine.

China ni miongoni mwa nchi zilizokataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW