SiasaChina
Xi Jinping ataka jeshi thabiti zaidi
13 Machi 2023Matangazo
Amesema hayo kwenye hotuba yake ya siku ya mwisho ya kongamano la kila mwaka la Bunge la Wananchi. Amesema "Ni lazima tuendeleze kwa kikamilifu, uboreshaji wa ulinzi wa taifa, wa vikosi vyetu na tujenge ukuta mkuu wa chuma, ambao unalinda kikamilifu uhuru wa taifa letu, usalama na masilahi yetu kimaendeleo.”
Bunge hilo liliidhinisha ongezeko la asilimia 7.2 kwenye bajeti kwa matumizi ya kijeshi, hiyo ikiwa ongezeko la juu kwa uwiano kuliko ongezeko lililopangwa la matumizi jumla.
Aidha alizungumzia pia mipango ya nchi yake ya kile alichokitaja kuwa ‘muungano' na Taiwan, japo alizungumza kwa sauti ya tahadhari.
Hakurudia kauli za awali kwamba China haitafutilia mbali uwezekano wa kutumia nguvu ya kijeshi kuhusu suala hilo.