1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi afanya mabadiliko makubwa baraza la mawaziri

12 Machi 2023

Baraza Kuu la Chama cha Kikomunisti cha China limeidhinisha baraza jipya la mawaziri linaoundwa na marafiki wa karibu wa Rais Xi Jinping katika uamuzi unaozidisha kumpa nguvu kiongozi huyo.

https://p.dw.com/p/4OZ5Y
China | Xi Jinping und Li Qiang | Archivbild 2022
Picha: NOEL CELIS/AFP

Mkutano huo uliwateua wajumbe waliobakia wa baraza jipya la mawaziri wakati ukielekea kuhitimisha kikao chake cha wiki nzima kinachofanyika kila mwaka jijini Beijing.

Wajumbe wapatao 3,000 waliidhinisha uteuzi wa mshirika wa muda mrefu wa Xi na mkuu wa zamani wa utumishi serikalini, Ding Xuexiang, kuwa makamu wa kwanza wa waziri mkuu, baada ya Li Qianga kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya siku ya Jumamosi (Machi 11).

Mtaalamu wa uchumi, He Lifeng, aliteuliwa kuwa makamu wa waziri mkuu mwenye dhamana ya kusimamia sera za uchumi na fedha, akichukuwa nafasi ya Liu He aliyekuwa akisimamia majadiliano ya biashara kati ya nchi yake na Marekani.

Soma zaidi: Bunge la umma wa China, limemteua Li Qiang kuwa waziri mkuu mpya
China yatetea mradi wake wa miundombinu

Jenetrali Li Shangfu, ambaye amewekewa vikwazo na Marekani, aliteuliwa kuwa waziri mpya wa ulinzi, baada ya kuongoza programu ya uendelezaji wa silaha kwenye Kamati Kuu ya Kijeshi.

China | Li Qiang
Waziri Mkuu mpya wa China, Li Qiang.Picha: GREG BAKER/AFP

Serikali ya Marekani chini ya Donald Trump ilimuwekea vikwazo Li na idara yake ya ukuzaji wa silaha mwaka 2018.

Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Wei Fengh, Li atakuwa mwakilishi pekee wa jeshi kwenye baraza jipya la mawaziri.

Mawaziri wa fedha, biashara, gavana benki kuu wabakia

Katika hatua ya kushangaza inayokusudiwa kuimarisha imani kwenye uchumi wa China, Xi aliwabakisha Liu Kun kwenye wizara ya fedha, Wang Wentao kwenye biashara na Yi Gang kuendelea na ugavana wa benki kuu.

Xi mwenye umri wa miaka 69 alikabidhiwa muhula wa tatu wa kuongoza chama na serikali siku ya Ijumaa (Machi 10), baada ya kuondosha ukomo wa umri na mihula katika mkutano mkuu wa chama uliofanyika mwezi Oktoba, akiimarisha nguvu zake kwenye taifa  hilo la pili kwa uchumi mkubwa duniani.

China | Nationaler Volkskongress
Wajumbe wa mkutano wa Baraza Kuu la chama cha Kikomunisti cha China.Picha: Noel Celis/AFP/Getty Images

Soma zaidi: Rais wa Iran ziarani China
China, EU zajenga matumaini ya kuikabili Marekani

Kwenye mkutano wa mwaka huu, wajumbe pia waliidhinisha mipango ya Xi kuhusu mabadiliko makubwa kwenye serikali katika miaka ya hivi karibuni. 

Mipango hiyo inajikita kwenye nafasi ya China kama kiongozi wa teknolojia na inahusisha kukata kiasi cha 5% ya nafasi za ajira serikalini.

Mageuzi makubwa yapitishwa

Mkutano huo wa Baraza Kuu la Chama cha Kikomunisti ulipangwa kukamilishwa siku ya Jumatatu (Machi 12) kwa mkutano wa waandishi wa habari na waziri mkuu mpya, Li Qiang. 

China | Nationaler Volkskongress
Rais Xi Jinping wa China.Picha: Mark R. Cristino/REUTERS

Soma zaidi: Rais Xi achaguliwa tena kwa muhula wa tatu kuongoza China

Miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuidhinisha ripoti za baraza la mawaziri lililomaliza muda wake na pia bajeti mpya inayohusisha ongezeko la 7.2% kwenye sekta ya ulinzi.

Kufuatia kukomeshwa kwa mkakati wa kupambana na janga la UVIKO-10 mnamo mwezi Disemba, serikali ya China inaamini kuwa uchumi wa taifa hilo utarejea kwenye hali yake ya kawaida mwaka huu na inatazamia ukuwaji wa takribani 5%.

Vyanzo: dpa, AFP