1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WTO yatamatisha mkutano bila kufikia makubaliano muhimu

Hawa Bihoga
2 Machi 2024

Mkutano wa shirika la Biashara diniani WTO uliokuwa unafanyika katika Umoja wa Falme za Kiarabu umemalizika leo Jumamosi, huku washiriki wakishindwa kufikia makubaliano juu ya masuala kadhaa muhimu.

https://p.dw.com/p/4d6LQ
Mkurugenzi wa Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala
Mkurugenzi wa Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-IwealaPicha: Li Xin/dpa/picture alliance

WTO ilichelewesha kilele cha mkutano huo mjini Abu Dhabi kwa zaidi ya siku moja wakati jumuiya hiyo ya kimataifa yenye wananchama 166, ikipambana kufikia muafaka juu ya sekta ya uvuvi, kilimo na masuala mengine muhimu. Makubaliano pekee yalioafikiwa ni ya kurefusha usitishaji wa kodi kwenye vyombo vya habari vya kidigitali.

Mkurugenzi wa Mkuu wa shirika hilo la Biashara Ngozi Okonjo-Iweala amesema mkutano huo umefanyika katika hali ambapo dunia imekumbwa na "mashaka makubwa" kuliko wakati wowote ule.

Soma pia:Mkutano wa WTO hauna dalili za makubaliano

Katika ufunguzi wa mkutano huo siku ya Jumatatu Ngozi hakugusia moja kwa moja mzozo wa Israel na Hamas, lakini alitaja usumbufu unaoendelea wa meli za kibiashara katika Bahari ya Shamu unaosababishwa na wapiganaji wa Kihouthi.