1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa WTO hauna dalili za makubaliano

1 Machi 2024

Majadiliano katika mkutano wa mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) mjini Abu Dhabi yamerefushwa kwa siku moja zaidi, huku shirika hilo likisema kikao cha mwisho kimecheleweshwa bila dalili za makubaliano.

https://p.dw.com/p/4d3v6
Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala.
Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala.Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

WTO ilisema hadi siku ya Alhamis (Februari 29) hakukuwa na dalili za mwafaka kuhusiana na mazungumzo ya kuweka sheria mpya za biashara duniani.

Katika baadhi ya vikao, majadiliano yaliendekea hadi usiku wa manane, maafisa wakitafuta makubaliano katika mabadiliko kadhaa katika sheria za biashara.

Soma zaidi:Nchi zinazolima pamba Afrika zaitaka WTO kusaka suluhisho 

Msemaji wa WTO, Ismaila Dieng, alisema mawaziri walikuwa wanafanya juhudi na wanapiga hatua.

Mkutano huo wa kila baada ya miaka miwili ulitaka yapatikane makubaliano ya kuondosha ruzuku za uvuvi na kuongeza muda wa malipo ya madeni katika ushuru wa biashara za kidijitali.

Afrika Kusini na India zinapinga hatua hiyo.

Tangazo la makubaliano ya mwisho liliahirishwa hadi Ijumaa (Machi 1).