1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSingapore

Wong aapishwa kama waziri mkuu wa nne wa Singapore

Sylvia Mwehozi
15 Mei 2024

Naibu kiongozi wa Singapore Lawrence Wong ameapishwa Jumatano kama waziri mkuu wa nne wa taifa hilo katika makabidhiano ya madaraka yaliyopangwa kwa uangalifu.

https://p.dw.com/p/4ftjb
Singapore| Lawrence Wong
Lawrence Wong aliyeapishwa kuiongoza SingaporePicha: Singapore Press/AP Photo/picture alliance

Naibu kiongozi wa Singapore Lawrence Wong ameapishwa Jumatano kama waziri mkuu wa nne wa taifa hilo katika makabidhiano ya madaraka yaliyopangwa kwa uangalifu ili kuhakikisha utulivu katika taifa hilo kitovu cha kibiashara katika kanda ya Asia.Waziri wa uchukuzi Singapore ajiuzulu kufuatia mashtaka nadra cha ufisadi

Wong, aliye na umri wa miaka 51, mchumi aliyefunzwa nchini Marekani, anamrithi Lee Hsien Loong ambaye alijiuzulu baada ya miongo miwili madarakani. Kuondoka kwa Lee kuliashiria mwisho wa nasaba ya familia iliyoongozwa na baba yake Lee Kuan Yew. Wong alikula kiapo chake katika hafla iliyoonyeshwa moja kwa moja na televisheni kya taifa.

Singapore | Lee Hsien Loong na Lawrence Wong
Lee Hsien Loong aliyejiuzulu(kushoto) akipeana mkono na Lawrence Wong Picha: Lim Yaohui/The Straits Times/SPH Media/REUTERS

Mfumo huo wa kubadilishana uongozi umeundwa kwa uangalifu na chama cha People's Action Party, mojawapo ya vyama vya siasa vilivyodumu kwa muda mrefu zaidi duniani na kujulikana kwa utawala wake safi na wenye ufanisi.Singapore yamnyonga mtuhumiwa wa dawa za kulevya

Wong, mtumishi wa umma aliyegeuka kuwa mwanasiasa, alijulikana wakati wa kuratibu mapambano yaliyopata mafanikio ya Singapore dhidi ya COVID-19.

"Kwa hakika nitajitahidi kuwa kiongozi mwenye nguvu, mkarimu na mwenye maamuzi. Na nitafanya niwezavyo kujenga Singapore ambapo kila mtu anaweza kutambua uwezo wake kamili," Wong alisema kwenye mtandao wa kijamii hapo awali

mwezi huu.

Singapore chini ya utawala wa Lee ilistawi na kuwa moja ya mataifa tajiri zaidi duniani, lakini pia ikawa moja ya mataifa ghali zaidi kuishi.