1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfsburg yashinda Bundesliga wanawake

Josephat Charo
17 Juni 2020

Wolfsburg imeshinda taji la nne mfululizo la ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga upande wa wanawake Jumatano (17.06.2020) kwa kuishinda Freiburg 2-0.

https://p.dw.com/p/3dvvK
Fußball Bundesliga | VfL Wolfsburg vs. SC Freiburg
Picha: Getty Images/M. Hitij

Ushindi huo unaiweka Wolfsburg ambao hawajapoteza mechi, na alama 58 baada ya mechi 20, ikiwa ni alama nane mbele ya timu iliyo katika nafasi ya pili, Bayern Munich, huku zikiwa zimesalia mechi mbili kucheza kabla msimu kukamilika.

Udhibiti wa Wolfsburg umejikita katika safu imara ya ulinzi ambayo imeruhusu magoli manene hadi sasa na safu madhubuti ya ushambuliaji ikiongozwa na mshambuliaji raia wa Denmark, Pernille Harder, ambaye mabao yake 26 ni sehemu ya jumla ya mabao 88 yaliyotimiwa kimyani na Wolfsburg msimu huu.

(reuters)