1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfowitz akubalika na Umoja wa Ulaya kuwa rais wa benki kuu ya dunia

30 Machi 2005

Mjini Brussel,Paul Wolfowitz amesema ana mipango ya kuunda tume ya kimataifa ya uongozi wa hadhi ya juu iwapo atadhibitishwa kuwa rais wa benki ya dunia

https://p.dw.com/p/CHhA
Paul Wolfowitz
Paul WolfowitzPicha: AP

Lakini hata hivyo amedinda kutoa ahadi yoyote baada ya mazungumzo na wakuu wa hazina wa Ulaya..

Matamshi yake hayo bwana Wolfowitz yamekuja baada ya Umoja wa Ulaya kutangaza azma ya kudhibiti cheo cha pili muhimu katika benki ya Dunia ambapo uteuzi wa Wolfowitz umekubwa na matatizo katika baadhi ya wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Uteuzi wa Worlfowitz ambaye kwa sasa ni naibu waziri wa usalama nchini Marekani na ambaye pia alikuwa nyuma ya Uvamizi wa Marekani nchini Iraq, umekosolewa vikali karibia katika kila pembe ya dunia.

Lakini licha ya hayo tume ya ulaya pamoja na viongozi wa umoja huo umzungumzia kuridhishwa kwao na ahadi aliyotoa Wolfowitz juu ya sera za kimaendeleo na hasa inayohusiana na masuala ya biashara na kupunguza umaskini .

Waziri wa misaada na maendeleo wa Ujerumani bibi Heidemarie Wieczoerek Zeul amesema wala ulaya hailengi juu ya kuhusika kwa Wolfowitz katika uvamizi wa Iraq lakini inachokijali hasa ni maono yake juu maendeleo.

Lakini kwa mujibu wa waziri wa maendeleo wa ubelgiji Armand de Decker amelezea wasiwasi walionao kwamba kila siku anachozungumzia Wolfowitz ni juu ya uchumi na maendeleo jambo ambalo Armand anasema halielewi na haelewi inamaanisha nini kwa kutaja uchumi na maendeleo.amesema kuna mabo fula fulani ambayo yanapasa kutatuliwa.

Wiki iliyopita Katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya viongozi wa Ulaya walionyesha ishara ya kuridhia uteuzi wa Wolfowitz na Marekani unaolenga kugharamia miradi ya maendeleo ya kipindi kirefu na kuyasaidia mataifa yanayoendelea.

Rais huyo mteule wa Benki kuu ya Dunia bwana Wolfowitz huenda akawaongoza watumishi elfu 10 wa Washington na ulimwengu kuangalia bajeti ya misaada ya kila mwaka ya dolla bilioni 9 amabazo zitasaidia mataifa maskini katika maendeleo.

Waziri mkuu wa Luxemboug Jean Claude Juncker anayeshikilia wadhifa wa wenyekiti wa zamu wa umoja wa ulaya amesema viongozi wa umoja huo walitaka mkutano na Wolfowitz kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo ya milenia yanapewa kipaumbele ambapo Wolfowitz atahitajika kufanyia mipango.

Malengo hayo ya maendeleo yamilenia ya Umoja wa Mataifa iliyoanzishwa mwezi septemba mwaka 2000 inalengo la kumaliza kwa kiwango cha nusu umaskini duniani ifikiapo mwaka 2015 na vilevile kupambana na maradhi kama vile Ukimwi na kifua kifuu na kurahisisha upatikanaji wa elimu.

Wakati wanadiplomasia wanasema ulaya inataka kupewa nafasi ya naibu wa rais wa benki kuu ya dunia,Ufaransa tayari imewasilisha majina mawili ya Jean Pierre Jouyet na Jean Pierre Landau kuchukua nafasi hiyo.

Ufaransa pia inataka naibu mwengine kutoka mataifa yanayoendelea.Naibu wa sasa wa rais wa Benki ya dunia ni Shengman Zhang kutoka china. kwa kawaida ilivyo desturi, ulaya inamchagua mkurugenzi mkuu wa IMF Na Marekani nayo inamteua rais wa benki kuu ya dunia.

Kimsingi sheria hiyo haijawahi kukiukwa tangu kuanzishwa kwa taasisi hizo mbili mnamo baada ya vita vya pili vya dunia. Baada ya kuongoza benki ya dunia kwa kipindi kirefu James Wolfensohn mwenye umri wa miaka 71 anatarajiwa kuondokea wadhifa huo mwezi Juni huku bodi ya benki kuu ikitaraji kumtaja nrithi wa mahala pa James hapo kesho.