1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Wizara ya afya Gaza: Watu 22,600 wameuwawa tangu Oktoba 7

5 Januari 2024

Wizara ya afya inayoendeshwa na Gaza imesema leo kuwa watu wapatao 22,600 wameuawa katika eneo la Palestina lililozingirwa tangu mzozo kati ya Israel na Hamas kuanza mnamo Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4auOD
Athari za mashambulizi ya anga huko Ukanda wa Gaza
Uharibifu unaofanywa na mashambulizi ya Israel Ukanda wa GazaPicha: Mohammed Dahman/AP Photo/picture alliance

Wizara hiyo imeeleza katika taarifa kuwa, watu 162 wamepoteza maisha na wengine 296 wamejeruhiwa huko Gaza katika saa 24 zilizopita.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa idadi jumla ya watu 57,910 wamejeruhiwa katika muda wa takriban miezi mitatu ya mapigano.