1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito watolewa Urusi kuchunguzwa kwa uhalifu wa kivita

10 Machi 2022

Urusi imeubadilisha msimamo wake kuhusu kulipuliwa kwa hospitali ya Ukraine katika mji wa Mariupol, kwa kutoa kauli za mchanganyiko ambazo zimepinga vikali na kutoa wito kwa Kremlin kutafuta ukweli wa kilichotokea. 

https://p.dw.com/p/48ImA
Ukraine zerstörte Geburtsklinik in Mariupol
Picha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Rais Vlodomyry Zelensky wa Ukraine amesema shambulizi hilo la bomu lilisababisha vifo vya watu watatu akiwemo mtoto mmoja, na kupinga kauli za Urusi kuwa hakukuwa na wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

Soma pia: Mawaziri wa mambo ya nje Urusi na Ukraine wakutana Uturuki

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov, amesema wanajeshi wa Urusi hawawalengi raia. Ikulu ya Kremlin imesema itachunguza tukio hilo. Peskov amesema wataliuliza jeshi kutoa taarifa Zaidi kuhusu kilichotokea kwa sababu serikali haina maelezo Zaidi.

Russland | Kreml-Sprecher Dmitri Peskow
Urusi imesema itachunguza shambulizi la hospitaliPicha: Shamil Zhumatov/AFP/Getty Images

Maafisa wengine wa Urusi waliushikilia msimamo mkali kwa kupinga uripuaji wa hospitali hiyo kuwa Habari bandia. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi Maria Zakharova, ameziita kauli hizo kuwa ni ugaidi wa habari.

Mashambulizi ya Urusi ya Mariupol leo yameuzuia msafara wa kibinaadam kufika katika mji huo unaokabiliwa na mashambulizi na hivyo kuathiri matumaini ya kuwahamisha wakaazi walionaswa na ambao wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula na bidhaa nyingine muhimu.

Petro Andrushenko, mshauri wa meya wa Mariupol amesema ndege za urusi zinazilenga njia zinazotumiwa kusafirisha msaada wa kiutu Pamoja na mabasi ambayo yanaandaliwa kwa ajili ya kuwasafirisha watu.

Kwingineko, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ameunga mkono wito wa kuwepo uchunguzi wa kimataifa dhidi ya Urusi wa uhalifu wa kivita kuhusu uvamizi wake wa Ukraine na kuwalipua raia, ikiwemo hospitali ya kina mama wajawazito.

Türkei | Treffen Sergei Lawrow und Dmytro Kuleba in Antalya
Wanadiplomasia wakuu wa Urusi na Ukraine walikutana UturukiPicha: Turkish Foreign Ministry/REUTERS

Akizungumza Pamoja na Rais wa Poland Andrzej Duda katika kikao cha waandishi Habari mjini Warsaw, ambako anaonyesha mshikamano wa Marekani kwa washirika wa NATO katika upande wa mashariki, Harris ameelezea hasira kuhusu mashambulizi hayo ya bomu hapo jana kwenye hospitali ya kina mama wajawazito. Kulikuwa na picha za wanawake waliojaa damu wakihamishwa.

Duda kwa upande wake amesema ni bayana kuwa Warusi wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine na kuongeza kuwa kwa mtazamo wake uvamizi huo una ishara za mauaji ya kimbari kwa sababu unalenga kuliangamiza taifa.

Soma pia: Urusi na Ukraine zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku nzima

Baadaye leo, Harris alitarajiwa kukutana na wakimbizi wa Ukrainwe waliokimbilia Poland tangu uvamizi huo uliopoanza. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa kuna zaidi ya wakimbizi milioni 1.4 walioingia Poland kati ya Zaidi ya milioni mbili ambao wameondoka Ukraine.

AFP/AP/DPA/Reuters