1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

William Ruto apiga kura katika eneo la Eldoret

9 Agosti 2022

Mgombea wa nafasi ya urais na naibu wa Rais Kenya, William Rutto kupitia muungano wa Kenya Kwanza, amepiga kura kijijini kwake katika eneo la Eldoret mapema Jumanne akiwa ameambatana na familia yake.

https://p.dw.com/p/4FJPd

Baada ya kukamilisha zoezi hilo alisema anaona uchaguzi huu ni wa tofauti kwani Wakenya wengi wamejitokeza ili kupigia kura sera na mpango ulio sahihi kwa muhula ujao. Kutaka kufahamu hali katika eneo hilo kwa sasa ikoje, Hawa Bihoga amezungumza na mwandishi wa habari Jeff Kirui akiwa katika eneo la Eldoret.