1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Watu 130,000 wanakabiliwa na njaa Pembe ya Afrika

10 Machi 2023

Shirika la Afya Duniani, WHO limeonya kuwa takribani watu 130,000 wanakabiliwa na baa la njaa katika Pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/4OWi9
Kenia Dürre l Leben im Dorf Parapul
Picha: Simon Maina/AFP

WHO imesema watu wapatao milioni 48 kwenye nchi za Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Uganda wanakabiliwa na viwango vya mzozo wa uhaba wa chakula.

Meneja matukio wa WHO katika  Pembe ya Afrika , Liesbeth Aelbrecht, amesema watu hao wanakabiliwa na njaa huku kifo kikiwanyemelea.

Aelbrecht amewaambia waandishi habari mjini Geneva kwa njia ya video kutoka Nairobi, kwamba kati ya watu 129,000, 96,000 wako Somalia na 33,000 Sudan Kusini.

Amesema maeneo mengi katika ukanda huo yanapambana na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, huku maeneo mengine yakiathiriwa kwa mafuriko. Kwa mujibu wa WHO, ongezeko la miripuko ya magonjwa limeshuhudiwa na idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo.