1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO kutumia chanjo ya majaribio dhidi ya Ebola DRC

Caro Robi
14 Mei 2018

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetoa idhini kwa chanjo ya majaribio kutumika kukabili Ebola nchini humo

https://p.dw.com/p/2xhXu
Kuba Ebola Trainingslager
Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Perez/Cubadebate

Shirika la afya duniani WHO limepewa idhini na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuingiza na kutumia chanjo ya majaribio ya kukabiliana na virusi vya Ebola nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dokta Tedros Adhanom Ghebreyesu amewaambia wanahabari kuwa sasa wana idhini ya kutumia chanjo hiyo na kuipongeza serikali ya Congo kwa kuchukua hatua za haraka kuudhibiti ugonjwa huo ambao umewaua wa tu 19 hadi sasa.

Wiki iliyopita, WHO iliripoti kuwa Ebola imezuka katika eneo la Bikoro lililoko katika jimbo la Equateur.  Takriban watu 393 wanafuatiliwa kuona kama waliambukizwa virusi hivyo na walioathiriwa 39.