1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaChina

WHO: China toweni takwimu ongezeko la maradhi ya kupumua

24 Novemba 2023

China imetahadharisha watu juu ya ongezeko la maradhi ya kupumua, nalo Shirika la Afya Ulimwenguni limeiomba nchi hiyo kutoa data kuhusu ugonjwa huo, likisema hakuna vimelea vipya au visivyo vya kawaida vilivyogunduliwa.

https://p.dw.com/p/4ZOta
Kiongozi | Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping Picha: GIANLUIGI GUERCIA/Pool via REUTERS

WHO imesema maeneo ya Kaskazini mwa China hasa jiji la Beijing na Liaoning yamerikodi ongezeko la ugonjwa unaofanana na homa ya mafua tangu katikati mwa Oktoba, ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka uliotangulia, huku ikiomba taarifa zaidi kuhusu hali hiyo.

Baraza la afya la taifa laChina limewaambia waandishi habari wiki iliyopita kwamaba ugonjwa huo wa kupumua ulitokana na kuondolewa kwa vizuwizi vya UVIKO-19 na mzunguko wa vimelea vinavyojulikana, ambavyo ni mafua na maambukizi maarugu ya bakteria wanaoathiria watoto, ikiwemo nimonia.

Soma zaidi: Wataalamu: Huenda kukazuka kirusi kipya cha Corona

Baraza hilo la taifa limesema ugonjwa wa mafua utaongezeka zaidi katika msimu huu wa baridi na huenda kukawa na maambukizi mengi katika baadhi ya maeneo katika siku zijazo. Ambapo pia wameonya juu ya hatari ya maambukizi mapya yaUviko-19.

Limesema 'maeneo yote yanapaswa kuimarisha utoaji wa taarifa juu ya magonjwa ya kuambukiza, ili kuhakikisha habari zinaripotiwa kwa usahihi na kwa wakati.

Suala hili limeibuka kufuatia Shirika la Afya Duniani kuiuliza China juu ya data walizorekodi katika 'Mpango wa ufuatiliaji magonjwa yamlipuko' kwenye makundi ya pneumonia isiyojulikana kwa watoto.

Uwazi bado changamoto kwa China

Wakati hilo liendelea, China na WHO bado zinakabiliwa na maswali yahusuyo hali ya uwazi wa kuripoti visa vya mapema zaidi kuhusu Uviko-19 ambayo iliibuka katikati mwa jiji la Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019.

Watu waliojikinga kwa barakoa wakiwa hospitali
Watu waliojikinga kwa barakoa wakiwa hospitaliPicha: JADE GAO/AFP

Mwezi huu mamlaka ilianza kutoa ushauri wa masuala ya afya, na kutahadharisha wananchi kusubiri kwa muda katika hospitali zenye watu wengi, lakini bado hazijaweka tahadhari kama ambazo iliweka kipindi cha janga Uviko-19, ikiwemo uvaaji wa  barakoa ama kufunga shule.

Soma zaidi: Wataalamu wa WHO watembelea maabara ya Wuhan

Kwa mujibu wa Bruce Thompson, Mkuu wa Shule ya Afya ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Melbourne, '"Data zilifaa kutolewa mapema sana, katika hatua hii, hakuna kitu cha kupendekeza na huenda hii ikawa ni kirusi kipya cha Uviko-19, jambo la msingi ni kuwa tumehakikishiwa kuwa taratibu za ufuatiliaji zinafanyiwa kazi, na hilo ni jambo zuri sana."

Baadhi ya wazazi hukoShanghai, wamesema hawakuwa na wasiwasi juu ya ongezeko la ugonjwa huo, wakati ukionekana kuenea kwa kasi pia walitaraji huenda ungeisha haraka.

Wazazi hao pia wamesema baridi ni hali ambayo hutokea maeneo mengi ulimwenguni, hivyo wanatumaini kuwa watu hawatakuwa na mtazamo tofauti kufuatia janga hilo bali watazingatia utafiti wa kisayansi. Pia wameeleza kua watoto wengi wanaougua sasa hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.