1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

White House: Zelensky kukutana na Biden mjini Washington

21 Desemba 2022

Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuwasili mjini Washington Jumatano hii, katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4LHcq
Ukraine Kiew | Pressekonferenz: Wolodymyr Selenskyj
Picha: Ukraine Presidency/Zuma/picture alliance

Ikulu ya White House imebaini kuwa Rais wa Marekani Joe Biden "anayo furaha ya kumkaribisha" Rais Zelensky katika Ikulu ya White House, ambaye baadaye atalihutubia Bunge la Marekani ili "kudhihirisha nguvu za pande mbili kwa ajili ya msaada kwa Ukraine.

Marekani inajiandaa kutoa kitita cha dola bilioni 45 za msaada wa dharura kwa Ukraine lakini pia ikijiandaa kupeleka mfumo wa kujilinda angani wa Patriot ili kuisaidia kupambana na mashambulizi ya Urusi.

Moscow kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Maria Zakharova imekemea hatua hiyo na kusema kipaumbele chake itakuwa kuiharibu mifumo hiyo.