1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

WFP yaanza kusambaza tena chakula Ethiopia

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Takriban asilimia 17 ya watu milioni 120 nchini Ethiopia wanategemea msaada wa chakula.

https://p.dw.com/p/4XLv2
Shirika la WFP limesema familia zinazoishi katika kambi za wakimbizi kwenye mikoa mitano wakiwemo wakimbizi wapya waliotoka Sudan wanapokea chakula cha msaada kwa mara ya kwanza tangu WFP lilipositisha usambazaji chakula mwezi Juni.
Shirika la WFP limesema familia zinazoishi katika kambi za wakimbizi kwenye mikoa mitano wakiwemo wakimbizi wapya waliotoka Sudan wanapokea chakula cha msaada kwa mara ya kwanza tangu WFP lilipositisha usambazaji chakula mwezi Juni.Picha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Shirika la Mpango wa Chula la Umoja wa Mataifa, WFP, limesema katika taarifa yake kwamba limeanza tena kusambaza chakula kwa wakimbizi wapatao 900,000 kote nchini Ethiopia baada ya kuimarisha utaritibu wa udhibiti kufuatia ripoti za wizi mkubwa wa misaada yake.

Shirika WFP lilisitisha usambazaji wa msaada wa chakula kote nchini Ethiopia mnamo mwezi Juni mwaka huu baada ya Marekani kutangaza ilikuwa inasitisha utoaji kutokana na msaada kuelekezwa kwingine.

Shirika la WFP na Shirika la misaada la Marekani USAID hayakutoa taarifa za kina kuhusu kuibwa kwa misaada kulikosababisha maamuzi yao.