1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yahofia vita vya Ukraine kusambaa

19 Januari 2024

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ameonya kuwa vita kati ya Urusi na Ukraine vinaweza kusambaa hadi kwenye nchi jirani.

https://p.dw.com/p/4bRgM
Kambi ya Augustdorf Ujerumani | Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius akiwa na afisa wa ngazi za juu wa jeshi Rommel Barracks
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius akiwa kwenye moja ya vifaru 14 aina ya Leopard 2.Panzer vilivyopelekwa nchini Ukraine kusaidia katika vita ambavyo Ujerumani sasa inaonyesha mashaka kwamba vitasambaa Picha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Pistorius ameliambia gazeti la Ujerumani la Tagesspiegel kwamba wanasikia vitisho karibu kila siku kutoka Urusi na hasa kitisho cha hivi karibuni dhidi ya mataifa ya kanda ya Baltiki.

Waziri huyo wa ulinzi amesisitiza kuwa wanapaswa kuimarisha haraka uwezo wao wa ulinzi kwa kuzingatia vitisho hivyo.

Pistorius amesema wanapaswa kuzingatia kwamba Rais wa Urusi Vladmir Putin anaweza siku moja kuzishambulia nchi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Amebainisha kuwa iwapo hilo litatokea, itakuwa kati ya miaka mitano hadi minane kuanzia sasa. Pistorius pia amekataa wito wa kuongeza msaada zaidi wa kijeshi wa Ujerumani kwenda Ukraine.