1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Waziri wa ulinzi wa Israel atishia kuivuruga vibaya Lebanon

27 Juni 2024

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema taifa lake halitaki vita na Lebanon, ingawa ameonya kuwa hawatasita kuishambulia vibaya ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa.

https://p.dw.com/p/4hZbj
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant akizungumza na wanajeshi wake walioko Rafah.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant akizungumza na wanajeshi wake walioko Rafah.Picha: Ariel Hermoni/Israel Mod/IMAGO

Gallant amewaambia waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Washington kwamba hawako tayari kwa vita, ingawa wamejiandaa kwa chochote kinachoweza kutokea.

Amesema Hezbollah wanatambua vizuri kwamba Israel inaweza kuleta uharibifu mkubwa huko Lebanon, kama watapigana vita.

Ameongeza kuwa jeshi la Israel lina na uwezo wa kuirejesha Lebanon kwenye "zama za mawe", katika vita dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

Maelfu ya watu kaskazini mwa Israel na kusini mwa Lebanon wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya Hezbollah na jeshi la Israel.