1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri wa ulinzi wa China Li Shangfu anazuru Urusi

14 Agosti 2023

Waziri wa ulinzi wa China Li Shangfu amekwenda nchini Urusi na Belarus katika hatua ya kuonesha kuyaunga mkono mataifa hayo mawili yaliyotengwa na nchi za Magharibi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4V8Vp
Singapur Shangri La Dialog | Li Shangfu
Picha: Vincent Thian/AP Photo/picture alliance

Waziri huyo wa ulinzi wa China ameondoka leo Jumatatu kuelekea katika ziara hiyo ya siku sita ambapo anatarajiwa kuhutubia katika mkutano kuhusu usalama wa Kimataifa na pia atakutana na viongozi wa ulinzi wa Urusi na mataifa mengine. Kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anatarajiwa kuzungumzia ajenda itakayojikita katika kile kinachoitwa nchi zenye idadi kubwa duniani kutafuta njia mbadala za maendeleo nje ya mifumo ya nchi za Kimagharibi. Wajumbe kutoka kiasi nchi 100 na mashirika manane ya kimataifa  wamealikwa kushiriki kwenye mkutano huo. Kushiriki kwa waziri wa ulinzi wa China katika mkutano huo kunadhihirisha  kiu ya China na Urusi ya ushirikiano wa sera zao za nje kwa lengo la kuhujumu mfumo wa demokrasia ya kiliberali inayoongozwa na nchi za Magharibi.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW