1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi Austin asitisha safari baada ya kulazwa

13 Februari 2024

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin ameahirisha safari ya yake kwenda Ubelgiji alikokuwa anapaswa kushiriki mikutano na mawaziri wengine wa ulinzi wa NATO.

https://p.dw.com/p/4cKm7
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin mjini Tel Aviv, Israel
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant katika Wizara ya Ulinzi ya Israeli huko Tel Aviv, Israeli Desemba 18, 2023.Picha: Violeta Santos Moura/REUTERS

Taarifa hiyo ni baada ya mkuu wa Pentagon kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi na kulazimika kukabidhi majukumu yake kwa naibu wake.Alipaswa kuanza safari kwa ajili ya mkutano wa NATO wa Alhamis lakini pia Jumatano ashiriki mkutano wa kujadili namna ya kuisaidia Ukraine katika makabiliano yake na uvamizi wa Urusi.Austin, mwenye umri wa miaka 70, Jumapili alipelekwa katika Kituo cha Matibabu cha Kijeshi cha Walter Reed kwa dalili zinazoashiria kuwa ni tatizo la kibofu. Inaelezwa pia kiongozi huyo hakuuweka hadharani upasuaji wa tezi dume aliofanyiwa Desemba na baadae Januari kulazwa hospitalini kukabiliana na matatizo yaliotokana na upasuaji huo.Bado haijaweza kujulikana mara moja ni kwa muda gani Waziri Austin atasalia hospitalini, lakini amekabidhi majukumu yake kwa Naibu Waziri wa Ulinzi Kathleen Hicks.