1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck ziarani Asia

20 Juni 2024

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck ambaye pia ni makamu wa Kansela wa Ujerumani anafanya ziara barani Asia.

https://p.dw.com/p/4hIRk
Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck
Ziara ya Habeck barani Asia itagusia masuala ya biashara, ulinzi wa mazingira na nishati.Picha: Michaela Küfner/DW

Waziri Habeck ataanza ziara yake ya kikazi ya siku tano nchini Korea Kusini ambako atakutana na Waziri Mkuu Han Duck Soo na Waziri wa Biashara Ahn Duk Geun.

Masuala atakayojadili na viongozi wa nchi hizo ni pamoja na masuala ya biashara, ulinzi wa mazingira na nishati. Waziri huyo wa Uchumi wa Ujerumani baada ya kuzuru Korea Kusini atakwenda China ambako anatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi.

Soma pia: Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck awasili Ukraine

Habeck anatazamiwa kuifafanua sera ya biashara ya Ujerumani nchini humo kuhusu ushuru ambao Umoja wa Ulaya uinataka kuweka katika uagizaji wa magari ya umeme kutoka China. China inapinga ushuru huo.