1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ndani wa Libya anusurika jaribio la mauaji

22 Februari 2021

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa amenusurika jaribio la mauaji dhidi yake, baada ya msafara wake kuvamiwa hapo jana kwenye barabara kuu mjini Tripoli.

https://p.dw.com/p/3phMu
Libyen | Von der UNO anerkannter Innenminister der Regierung des Nationalen Abkommens (GNA) | Fathi Bashagha
Picha: Getty Images/AFP/M. Turkia

Mashambulizi hayo dhidi ya Fathi Bashagha yalimjeruhi mmoja wa walinzi wake, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya, Ami Al-Hashmi. 

Wizara yake ya mambo ya ndani inasema Bashagha alikuwa akirejea nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Janzour wakati watu wenye silaha walipowavamia. 

Mapema hapo jana, Bashagha alikutana na mkuu wa shirika la mafuta la Libya, Mustafa Sanalla, kuzungumzia usalama kwenye visima na mitambo ya kusafishia mafuta na jinsi ya kulifanya shirika hilo kuwa huru na kuweza kugawanya utajiri wa mafuta kwa Walibya wote. 

Jaribio hilo la mauaji ni pigo kwa serikali mpya iliyoundwa kuiunganisha nchi kuelekea uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.