1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Waziri Sergei Lavrov wa Urusi afanya ziara nchini Mali

7 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, anafanya ziara nchini Mali.

https://p.dw.com/p/4NBGT
Minister Sergey Lavrov trifft  Esteban Lazo Hernandez
Picha: Russian Foreign Ministry Press Service/AP/picture alliance

Lavrov atafanya mazungumzo na viongozi wa kijeshi wa Mali wanaotafuta msaada wa Urusi katika kukabiliana na waasi wa makundi ya watu wenye siasa kali yanayosumbua nchi hiyo kwa muda mrefu. 

Lavrov, alipowasili mjini Bamako asubuhi ya leo, akitokea kwenye ziara ya nchini Iraq  alipokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop.

Ziara ya kiongozi huyo wa Urusi ni ya tatu barani Afrika tangu mwezi Julai mwaka uliopita katika juhudi za kuongeza ushawishi wa Urusi kwenye bara hilo huku ikiwa imetengwa kimataifa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.