1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Baerbock aihimiza China kuiambia Urusi isitishe vita

14 Aprili 2023

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock anayeitembelea China ameitolea mwito Beijing kusaidia kumaliza vita vinavyoendelea nchini Ukraine akisema hakuna taifa lenye ushawishi kwa Urusi kuishinda China

https://p.dw.com/p/4Q3b3
China Aussenministerin Annalena Baerbock |  Qin Gang
Picha: Suo Takekuma/Pool via REUTERS

Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani ametoa matamshi hayo baada ya kukutana na mwenzake wa China Qin Gang ambapo wamejadili pamoja na mambo mengine, suala la haki za binadamu na kutanuka kwa mvutano juu ya kisiwa cha Taiwan.

Soma pia: Nchini China, Baerbock asema maoni ya Macron ni ya Ulaya

Ama kuhusu dhima ya China katika kukomesha vita nchini Ukraine Bibi Baerbock amesema; "Ninatumia ziara yangu pia kuirai China, kama mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kupigania amani ulimwenguni na kusaidia kuhakkisha kwamba vita vya kutisha vya Urusi vinafikia mwisho"

Katika miezi ya karibuni China imechukua jukumu la kutaka kuwa mpatanishi wa mzozo wa Ukraine lakini mataifa ya magharibi yana mashaka na dhamira ya Beijing iliyo mshirika mkubwa wa Moscow.