1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani abanwa zaidi juu utoaji wa vibali.

16 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFdH

Vyama vinanvyo tawala hapa nchini Ujerumani vimekataa matakwa ya vyama vya upinzani juu ya waziri wa mambo ya nje bwana Yoschka Fischer,

kufikishwa mbele ya kamati ya uchunguzi mapema kabla ya ilivyo pangwa.

Makatibu wakuu wa vyama vya upinzani wanataka bwana Fischer afikishwe mbele ya kamati hiyo kabla ya uchaguzi wa majimbo utakao fanyika mwezi mei.

Waziri Fischer anakabiliwa na mgogoro wa kisiasa kutokana na wizara yake kuhusika na taratibu legevu zilizotumiwa katika kutoa vibali vya kuhamia nchini Ujerumani ambapo maalfu ya watu kutoka nchi za Ulaya Mashariki ikiwa ni pamoja na makahaba na wahalifu waliweza kuingia hapa Ujerumani kirahisi.

Wakati huo huo waziri wa Yoshcka Fischer leo amekutana na mfani wake wa Iran Kamal Charrasi mjini Berlin ili kuzungumzia juu ya mzozo unaotokana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Ujerumani pamoja na nchi zingine za umoja wa Ulaya zinafanya juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kuishawishi Iran iache mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium ambayo ni nyenzo muhimu katika utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la nishati ya nyuklia bwana Mohamed El Baradei amesema kwamba hadi sasa hajaona ushahidi wowote juu ya Iran kuwa na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia.