1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Takeshi Iwaya, kwenda China

24 Desemba 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Japan Takeshi Iwaya anatarajiwa kuitembelea China kesho Jumatano kwa mazungumzo na mwenzake wa China Wang Yi

https://p.dw.com/p/4oXqw
Japan |Takeshi Iwaya
Kushoto: Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Takeshi IwayaPicha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Japan imekiri uwepo wa changamoto na wasiwasi kuhusu mahusiano kati yake na China.

Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Iwaya nchini China tangu kuchaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Japan mapema mwaka huu.

Aliwaambia waandishi habari mjini Tokyo kwamba China inawakilisha mahusiano muhimu sana kwa taifa lake huku akisema kwamba mataifa hayo mawili yanaweza kufanya mambo makubwa pamoja na kwamba kuna changamozo na wasiwasi.

China na Japan ni washirika wakubwa wa biashara lakini mahusiano kati ya nchi hizo yameingia mikwaruzano iliyosababishwa na mvutano wa umiliki wa maeneo ya kikanda na kuoneshana nguvu za kijeshi kumesambaratisha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika miaka ya hivi karibuni.