1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiNigeria

Waziri wa kupambana na umasikini afutwa kazi Nigeria

9 Januari 2024

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, amemsimamisha kazi waziri wake anayehusika na masuala ya msaada na kupambana na umasikini.

https://p.dw.com/p/4b1UK
Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Ubale Musa/DW

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, amemsimamisha kazi  waziri wake anayehusika na masuala ya msaada na kupambana na umasikini, Beta Edu, kufuatia kadhia ya kufanya miamala ya fedha za kusimamia miradi ya masuala ya ustawi wa jamii kwa kupitia akaunti yake binafsi.

Waziri huyo ameondolewa kazini mara moja huku shirika la kupambana na rushwa nchini Nigeria likifanya uchunguzi wa kina kufuatilia miamala yote iliyofanywa katika wizara hiyo.

Rais Bola Tinubu aliyeingia madarakani mwaka jana aliahidi kupambana na rushwa iliyopindukia katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW