1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaQatar

Waziri wa kazi wa Qatar ateuliwa kuongoza mkutano wa ILO

5 Juni 2023

Waziri wa kazi wa Qatar ameteuliwa kuongoza mkutano wa kupitisha maamuzi wa kila mwaka wa Shirika la Kazi Duniani, ILO.

https://p.dw.com/p/4SDVU
Schweiz Genf | 110. Sitzung der Internationalen Arbeitsorganisation
Picha: Crozet/Pouteau/Albouy/ILO

Licha ya kusikika sauti za ukosoaji kutoka kwa baadhi ya vyama vya wafanyakazi juu ya mashaka yaliyopo kuhusu hali ya mazingira ya kufanya kazi nchini Qatar.

Mataifa ya Asia na Pasifiki ambayo mwaka huu yalikuwa na jukumu la kupokezana kikanda, la kuchagua rais wa mkutano huo wa wiki mbili wa kimataifa wa ILO, yalimpendekeza Ali Bin Al- Marri.

Soma pia: Mataifa ya Kiarabu yaujadili mgogoro wa Syria

Kawaida uteuzi huo huidhinishwa kwa makubaliano ya pamoja ingawa mwaka huu baadhi ya vyama vya wafanyakazi vilitaka ufanyike mchakato wa kupigwa kura kufuatia mashaka kuhusu hali ya mazingira ya wafanykazi nchini Qatar, iliyozusha maswali kuhusu uthabiti wa kuteuliwa waziri huyo wa Qatar kuongoza mkutano huo wa kimataifa.