1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa fedha wa Ujerumani amewasili mjini Keiv.

14 Agosti 2023

Waziri wa fedha wa Ujerumani Christian Lindner amewasili mjini Keiv,Ukraine kwaajili ya mazungumzo ya kisiasa na viongozi nchini humo,ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika taifa hilo tangu Urusi ilipofanya uvamizi.

https://p.dw.com/p/4V8Vq
Ukraine | Christian Lindner in Kiew
Picha: Thomas Imo/photothek/IMAGO

Serikali ya Ukraine imekuwa ikiishinikiza Ujerumani kuipatia makombora yenye uwezo mkubwa ya Taurus,kwaajili ya kujilinda dhidi ya uvamizi huo wa Urusi. Ziara hiyo ya Lindner mjini Kiev imekuja wakati Urusi imezidisha mashambulio yake dhidi ya Ukraine. Jeshi la Ukraine limesema hii leo Urusi imefanya msururu wa mashambulio ya makombora dhidi ya eneo la Kusini katika pwani ya bahari nyeusi.Kamandi ya kijeshi ya Ukraine katika eneo hilo imefahamisha kwamba mashambulio matatu yamefanyika katika mji wa Odessa usiku wa kuamkia leo lakini wanajeshi wa kikosi cha wanaanga waliyazuia mashambulio yote,ingawa jengo la bweni ya wanafunzi na duka yaliharibiwa katikati ya mji huo wa Odessa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW