1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri mkuu wa zamani Thailand anatarajiwa kurejea nchini.

21 Agosti 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Thailand, Thaksin Shinawatra, anatarajiwa kurejea nchini humo kesho kutoka uhamishoni alikokimbilia.

https://p.dw.com/p/4VOY2
Ehemaliger thailändischer Premierminister Thaksin Shinawatra
Picha: picture alliance/Kyodo

Hatua hiyo inatishia kusababisha kuzuka upya ukosefu wa uthabiti nchini humo katika siku ambapo bunge litapiga kura ya kumchagua waziri mkuu mpya baada ya kushuhudiwa miezi mitatu ya mkwamo wa kisiasa, ulioifanya nchi hiyo kukaa bila ya kiongozi.Thaksin, mwenye umri wa miaka 74, anarejea nyumbani baada ya kukimbilia uhamishoni kwa miaka 15 kufuatia kuandamwa na mashtaka ya uhalifu ambayo anadai yalichochewa kisiasa. Mwanasiasa huyo anaungwa mkono na wananchi wengi wa vijijini, ambao maisha yao yalibadilika kutokana na sera zake mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini anapingwa na wanaoliunga mkono jeshi na utawala wa kifalme.