1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan afikishwa tena mahakamani

12 Mei 2023

Waziri mkuu wa zamani nchini Pakistan, Imran Khan amefikishwa tena mahakamani leo Ijumaa chini ya ulinzi mkali, kusikiliza uamuzi utakaotolewa na mahakama kuu kuhusu ikiwa ataepuka kukamatwa tena au kurudishwa kizuizini

https://p.dw.com/p/4RGoT
Politik in Pakistan
Picha: K.M. Chaudary/AP/dpa/picture alliance

Uamuzi huo unaiweka serikali ya nchi hiyo na wafuasi wa kiongozi huyo katika nafasi ngumu baada ya siku kadhaa za kushuhudiwa makabiliano. Kikao cha leo cha mahakama ni sehemu ya mchakato mrefu wa kisheria. Jana Alhamisi mahakama ya juu kabisa  ya nchi hiyo ilitowa uamuzi ikisema kwamba kukamatwa kwa Imran Khan kilikuwa kitendo kilichokwenda kinyume na sheria lakini ikaitaka mahakama ya juu ya Islamabad kutafakari uamuzi wake wa mwanzo wa kuunga mkono kukamatwa huko kwa Khan. Mahakama ya juu pia imesema itaheshimu uamuzi utakaochukuliwa leo na mahakama kuu ya Islamabad. Kwa upande mwingine serikali imesema itamkamata kiongozi huyo haraka ikiwa mahakama kuu ya Islamabad itamnyima dhamana ya kuachiliwa.