1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Waziri Mkuu wa zamani wa Italia yuko mahututi

5 Aprili 2023

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi, ambaye alichangia pakubwa katika siasa za taifa lake kwa miongo mingi, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na matatizo ya moyo.

https://p.dw.com/p/4PjwE
Italien I Silvio Berlusconi
Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi Picha: Andrew Medichini/AP/picture alliance

Seneta huyo mwenye umri wa miaka 86 na tajiri wa vyombo vya habari, ambaye amekuwa akilazwa na kutoka hospitali katika miaka ya karibuni, yuko katika hospitali ya San Raffaele mjini Milan.

Shirika la habari la Italia Ansa limesema alilazwa hospitali mapema leo na kuwa hali yake ya sasa inatengemaa.

Berlusconi, kiongozi bilionea wa chama cha siasa za mrengo wa kulia cha Forza nchini Italia, alikaa katika hospitali hiyo kwa siku nne mwezi uliopita kwa kile ripoti za vyombo vya habari vya Italia zilisema matatizo ya moyo kabla ya kuruhusiwa kuondoka mnamo Machi 30.