1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Scott Morrison wa Australia akosolewa kwa kujipatia vyeo

30 Novemba 2022

Scott Morrison hii leo amekuwa waziri mkuu wa kwanza wa zamani wa Australia kupigiwa kura ya karipio na bunge la nchi hiyo, kutokana na kushindwa kwake kuweka wazi teuzi za ziada za uwaziri.

https://p.dw.com/p/4KHp1
Misstrauensvotum gegen Australiens Ex-Premier Morrison
Picha: Lukas Coch/AAP/dpa/picture alliance

Wakati wa janga la Uviko-19, mwanasiasa huyo wa kihafidhina alijipa nyadhifa tano nyingine za uwaziri mbali ya nafasi yake kama waziri mkuu, bila kuufahamisha umma au baraza lake.

Tangu kufichuliwa kwa habari hizo mwezi Agosti, kumekuwa na miito ya mara kwa mara kwa Morrison kuomba radhi hadharani na kujiuzulu ubunge.

Hii leo bunge limepitisha azimio la kumkosoa vikali mwanasiasa huyo kwa kura 86 dhidi ya 50.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Australia, kura hiyo haina uzito wowote kisheria, lakini ilikuwa pia ya kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa zamani wa Australia kukaripiwa vikali.