1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Waziri Mkuu wa Urusi kufanya ziara nchini China

19 Mei 2023

Waziri Mkuu wa Urusi Mikhail Mishustin, anatarajiwa kusafiri kuelekea Beijing tarehe 23 na 24 kwa mazungumzo na viongozi wa serikali ya China akiwemo Rais Xi Jinping pamoja na Waziri Mkuu, Li Qiang.

https://p.dw.com/p/4RahN
Waziri Mkuu wa Urusi, Mikhail Mishustin
Waziri Mkuu wa Urusi, Mikhail MishustinPicha: Grigory Sysoev/SNA/IMAGO

Katika ziara hiyo, Mishustin atahudhuria mkutano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili mjini Shanghai, utakaowajumuisha wawakilishi wa nchi zote mbili pamoja na makampuni makubwa.

Masuala muhimu ya ushirikiano wa China na Urusi, upande wa biashara, uchumi, nishati, kilimo na miundombinu pia yatazungumziwa.

China ambaye ni mshirika mkubwa wa Urusi imejizuwia kuiwekea Urusi vikwazo kinyume na mataifa mengine yaliyo na nguvu duniani.

Uongozi wa China haujavikosoa hadharani vita vya Urusi nchini Ukraine, na badala yake imeamua kuwa mpatanishi wa pande hizo mbili zinazozozana.