1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUreno

Waziri Mkuu wa Ureno kujiuzulu kufuatia kashfa ya ufisadi?

7 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa Jumanne anatarajiwa kulihutubia taifa na huenda akajiuzulu baada ya kuhususishwa katika kashfa ya rushwa na ufisadi katika utoaji wa kandarasi katika mikataba ya nishati.

https://p.dw.com/p/4YWa5
Ureno | Uchaguzi wa bunge| Waziri Mkuu Antonio Costa
Waziri Mkuu wa Ureno Antonio CostaPicha: Armando Franca/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ureno, waziri Costa tayari amefanya mazungumzo na rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa.

Waendesha mashtaka tayari wamemtia kizuizini waziri wa miundombinu Joao Galamba na afisa mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu kwa madai ya ukiukwaji wa sheria katika uchunguzi unaoendelea kuhusu miradi ya nishati za lithium na hidrojeni.