1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Rishi Sunak azuru Ireland Kaskazini

28 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amezuru Ireland Kaskazini ili kuvishawishi vyama vya wafanyakazi vinavyoegemea Uingereza kuunga mkono muafaka aliosaini na Umoja wa Ulaya

https://p.dw.com/p/4O57n
UK Rishi Sunak  in Nordirland
Picha: Liam McBurney/AP/picture alliance

Sunak na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen waliuita mpango huo mpya jana kuwa ni "sura mpya" katika mahusiano baada ya miaka kadhaa ya mivutano ya Brexit. Wakati mpango huo umepokelewa vyema kwa ujumla, bado haujapata uungwaji mkono wa Chama cha Democratic Unionist - DUP, chama kikubwa zaidi Ireland Kaskazini kinachoegemea Uingereza, ambao unahitajika ili kuanza tena kugawana madaraka katika mkoa huo.

Mkuu wa chama hicho Jeffrey Donaldson amesema watatathmini kama makubaliano hayo yalitimiza vigezo vyao vya kurejea katika Bunge la Ireland Kaskazini.