1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Waziri Mkuu wa Uingereza awasili Ukraine

12 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak yuko nchini Ukraine kuzindua awamu mpya ya msaada kwa ajili ya Ukraine na kuongeza ufadhili wa kijeshi kwa mwaka huu wa fedha hadi pauni bilioni 2.5.

https://p.dw.com/p/4bA4b
Ukraine | Kuwasili kwa Rishi Sunak Kyiv.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwasili mjini Kyiv kwa njia ya treni, kukutana na Rais Volodymyr Zelenskiy, Januari 12, 2024.Picha: Stefan Rousseau/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak yuko ziarani nchini Ukraine kuzindua awamu mpya ya msaada kwa ajili ya Ukraine na kuongeza ufadhili wa kijeshi kwa mwaka huu wa fedha hadi pauni bilioni 2.5.

Ofisi ya Sunak imesema fedha hizo ni ongezeko la pauni milioni 200 katika kipindi cha miaka miwili, na itahakikisha dhamira kubwa zaidi kuwahi kutokea ya kuipatia droni serikali ya Ukraine.

Soma pia:Sunak: Uingereza itasimama kidete na Ukraine 

Sunak pia anatarajiwa kusaini makubaliano ya kihistoria ya ushirikiano wa usalama na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky. Ufadhili huo wa ziada utajumuisha manunuzi ya makombora ya masafa marefu, mfumo wa ulinzi wa anga, na usalama baharini.

Waziri huyo mkuu wa Uingereza pia anatarajiwa kukutana na wafanyakazi wa huduma za dharura ambao wanatoa huduma baada ya mashambulizi ya anga ya Urusi.